Pambazuko FM Radio

Kilombero festival kuvutia uwekezajiKilombero

8 December 2024, 5:45 pm

Na Katalina Liombechi

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya ametumia tamasha la Kilombero(Kilombero Festival)kuwaita wawekezaji kuwekeza kimkakati katika Wilaya hiyo yenye utajiri na urithi wa pekee kutokana na uwepo wa fursa nyingi za aina yake.

Akizundua Tamasha hilo Kyobya amesema Kilombero inajivunia vivituo na Fursa mbalimbali za Kiuchumi kutokana na bonde hilo kuwa na fursa nyingi za utalii na ni bonde zuri kwa shghuli za Kilimo.

Picha ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya akitembelea Mabanda Tamasha la kilombero Festival(Picha na Katalina Liombechi)

Hata hivyo kufuatia uzinduzi wa Tamasha hilo ambao umefanyika Dec 7,2024 wanachi waliohudhuria katika viwanja vya CCM Tangani Ifakara kushuhudiawameelezea kuzutiwa na ubunifu huo huku wakitamani liwe endelevu.

Sauti za baadhi ya wakazi wa Ifakara Wilayani Kilombero

African Wildlife Foundation ni miongoni mwa wadau wa Uhifadhi walioshiriki Tamasha hilo ambapo kupitia kwa Mchumi kilimo Alexander Mpwaga wameonyesha na kuhamasisha uwekezaji unaojali bonde la kilombero,namna wanavokuza uchumi wa watu,kushirikana na wadau wengine kufanya uhifadhi endelevu huku akitoa wito kwa jamii kuheshimu matumizi bora ya ardhi.

Picha ya Alexander Mpwaga Mchumi Kilimo AWF akimpatia elimu mteja aliyetembelea banda hilo(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Alexander Mpwaga Mchumi Kilimo AWF

Tamasha la namna hiyo lililobeba ajenda za utalii na uhifadhi endelevu katika Wilaya ya Kilombero ni Mara ya kwanza kufanyika na kwamba kwasasa litakuwa likifanyika kila mwaka ili kukuza maendeleo na Fursa zinazopatikana katika Wilaya ya Kilombero.