Mkoani FM

Wanahabari Pemba watakiwa kufanya uchechemuzi wa sheria za habari

25 July 2025, 3:26 pm

“Waandishi endeleeni kufanya uchehemuzi wa sheria za habari ili wenye mamlaka waweze kutunga sheria mpya za habari zitakazo toa uhuru kwa wanahabari kufanya kazi zao”

Khadija Ali Yussuf

Waandishi wa habari kisiwani Pemba wametakiwa kuendelea kufanya uchechemuzi wa sheria za habari ili kupatikana kwa sheria mpya za habari Zanzibar.

Akizungumza katika ukumbi wa TAMWA Ofisi za Pemba msimamzi wa mradi Zaina Abdallah Mzee wakati wa kikao cha mrejesho wa mradi wa mapitio ya sheria za uhuru wa kujielezea, amesema licha ya kuwa mradi huo umefika mwisho ni muhimu kwa waandishi hao kuendelea kupigia chapuo ili vyombo husika viweze kutilia mkazo kupatikana sheria mpya.

 Kwa upande wake Afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka TAMWA Zanzibar Moh’d Khatib amesema bila kuangalia madhaifu ya sheria yaliyomo katika sheria hizo basi uhuru wa habari hautopatikana.

Ameongeza kwa kusema ipo haja kwa waandishi kuengeza nguvu za ziada kwa kushirikiana na wadau wa habari ili sheria hiyo iweze kupatikana.

Nao waandishi walioshiriki mafunzo hayo, wameishukuri TAMWA kwa mafunzo waliyowapatia na kuahidi kuendelea kufanya uchechemuzi ili sheria mpya iweze kupatikana.

Mkutano huo wa siku uloiandaliwa na TAMWA Zanzibar yamewakutanisha waaandishi waliopata mafunzo ya uchechemuzi wa sheria ya habari wamiliki wa vyombo vya habar pamoja na wahariri yamefanyika katika Ofisi za TAMWA Pemba.