Mkoani FM

Makoongwe waomba huduma bora za kijamii

12 September 2023, 9:23 pm

katibu wa Mbunge Mariam Said Khamis( Picha na Khatibu Nahoda)

Wananchi wa kisiwa cha Makoongwe kinachopatikana mkoa wa Kaskazini Pemba wameomba kupatiwa huduma mbalimbali za kijamii kutokana na huduma hizo kukosekana muda mrefu na kumtaka mbunge wa jimbo la Mkoani kutimiza wajibu wake kwao.

Na Khatib Juma

Wananchi wa shehia ya Makoongwe Jimbo la Mkoani kisiwani Pemba wameiomba serikali kupitia jimbo kuboreshewa huduma za kijamii zinazowakabili ili kukua kimaendeleo.

Wakizungumza katika mkutano na uongozi wa jimbo hilo baada ya kufika katika shehia yao wamesema kuna changamoto ambazo ni kikwazo kufikia maendeleo kama shehia zingine.

Mwananchi Mkubwa Ali Yussuf amesema changamoto hizo ni pamoja na uhaba na uchakavu wa mabanda ya kusomea  kwani hulazimika banda moja kutumiwa na wanafunzi wa mabanda mawili tofauti jambo ambalo linakosesha ufanisi wa ufundishaji na watoto kufaulu vizuri.

Safia Ali Mussa amesema kukosekana kwa huduma ya maji katika vyoo vya skuli ya Makoongwe limekuwa tatizo la muda mrefu hivyo huwalazimu wanafunzi kwenda kuomba vyoo nje ya skuli na wakati mwingine kujisaidia vichakani jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao hasa kwa wanafunzi wa kike.

Khamis Said Masoud na Salama Bakar Haji wamesema  tatizo la kivuko hukosekana kusafirisha wagonjwa kutoka Makoongwe kwenda hospitali ya Abdalla Mzee hususani akina mama wajawazito kwani hakuna kituo cha mama na mtoto hivyo  wameomba kupatiwa kituo cha mama na mtoto ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza.

Akizungumza wakati wa kutoa ufafanuzi juu ya changamoto zilizo wasilishwa katibu wa Mbunge Mariam Said Khamis kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la Mkoani Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ameahidi kuzipeleka chamgamoto hizo kwa Mbunge kama zilivyo ili zipatiwe ufumbuzi.

Aidha amewaomba wananchi hao kuwendelea kua na imani na viongozi pamoja na kuwaunga mkono juhudi za utendaji kazi wao ili waweze kitekeleza majukum yao kama ilani ya chama cha mapinduzi inavyoelekeza.

Mapema akizungumza katika mkutano huo Diwani wa Wadi ya Michenzani Mashavuu Amour, amewambia wananchi hao viongozi wameomba ridha ya kuongoza kwa lengo la kuwaletea maendeleo na sio kujifaidisha hivyo waendelee kuwapa imani na kuwaunga mkono ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Mara baada ya kumaliza kwa mkutano huo katibu huyo wa mbunge pamoja na viongozi wa chama wa jimbo la mkoani wamefanya ziara ya kukagua mashine ya kukobolea mpunga iliyotolewa na Profesa Mbarawa ambayo kwa muda mrefu ilishindwa kutoa huduma kutokana na kukosa umeme wa uhakika.