Mkoani FM

Uchumi wa buluu kuwainua vijana Pemba

8 September 2023, 9:40 am

Afisa mdhamini Wizara ya uchumi wa Buluu Mohd Ali wakivuu KAA ni moja ya kitoeleo kinchopatikana Bharini (Picha Fatma Hamad)

Vijana wanatakiwa wasisubiri ajira serikalini bali wajishugulishe kwenye shuguli mbali mbali zikiwemo fursa za uchumi buluu kwa kujiunga kwenye vikundi vya ujasiariamali ili waweze kujiengezea kipato

Vijana wameonywa  kuepuka kukaa katika vigenge viovu ,na badala yake wajiunge  na vikundi  vya ushirika,  ili waweze kujipatia kipato cha halali.

Ushauri huo umetolewa na katibu wa kikundi cha ushirika  mapambano coperetive kinacho jishuhulisha na ufugaji wa Samaki, kaa, kamba  na mboga mboga  Bishara Muhammed Musa mbele ya  wanakikundi hao,  mara baada ya kutembelewa na wajumbe kutoka wizara ya uchumi wa Buluu na shirika la  International  Union for conservation of Nature  [IUCN] kutoka Tanzania bara huko Sizini wilaya ya Miheweni Mkoa wa Kaskazi Pemba.

Ameeleza wakati umefika  kwa vijana  kuwamka na kujiajiri wenyewe, na sio kukaa tu vigengeni na kusubiri ajira Serikalini.

Aidha  alieleza kuwa  sera ya Serikali  ya mapinduzi ya Zanzibar ya uchumi wa buluu  unaelekeza zaidi kwenye bahari, hivvyo  aliwasisitiza  viajana hao   kukiendeleza kikundi chao kwa juhudi zote, jambo ambalo litawawezesha kupata ursa mbali mbali za kimaendeleo.

Mapema mwanakikundi Khadija  Ali  Juma alieleza kuwa ameamua kujiunga kwenye kikundi  cha ujasiriamali, ili aweze kujipatia kipato  kitakacho msaidia katika familia yake.

Aidha amesema mafanikio hayaji tu kama ndoto, hivyo ni vyema kuwa wavumilivu kupitia changamoto zinazowatokezea ili waweze kukiikisha mbele kikundi chao.

Mwenyye kiti wa kikundi hicho Khalfan Hamad Khalfan alieleza kuwa  matarajio yao ni kuhakikisha wamekuwa wazalishaji wakubwa  wa mazao ya baharini.

Hivyo aliomba wizara ya uchumi wa buluu kujitokeza na kuwaunga mkono vikundi ambavyo vimewekeza juhudi zao kwenye maeneo ya bahari, ili waweze kunufaika na fursa zilizomo,  ndani ya  sera ya uchumi wa buluu.

 Nae  afisa kutoka wizaa ya uchumi wa buluu Pemba Mohd Ali  pamoja na wajumbe kutoka  shirika la International  Union for conservation of Nature  [IUCN] ni kuangalia maendeleo yao, na kuelewa changamoto zinazo wakabili  wanakikundi hao  na kuweza kutatuliwa.

Kkikundi hicho ambacho kinawanachama 17 wanaume 8, na wanawake 9, ambacho kilianza rasmi mwaka 2013.