Mkoani FM

Wananchi Pemba wanatakiwakuandika urithi ili kuepuka migogoro

28 August 2022, 2:45 pm

 

Wananchi kisiswani Pemba wameshauriwa kuzingatia suala la mirathi mara tu baada ya mzazi kufariki ilikuepusha migogoro isiyo ya lazima katika familiya.

Kauli hizo zimetolewa na  zulekha suleimn sheha na Sharifa Shaban Hamad wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi amesema wanawake wamekua wahanga wakuu katika kukosa haki yao baada ya mzazi kufariki hali inayopolekea migogoro isiyoisha kwa familia na hata jamii kiujumla.

..

Wameongeza mwanamke anapodai haki ya urithi wake huonekana hana mamlaka na mali iliyoachwa na marehemu jambo ambalo sio sahihi katika dini, na linanyima fursa ya miradhi kwa jinsia hiyo.

 

Georgina lund msaidizi wa usimamizi wa kumbukumbu kutoka taasisi ya Foundation for Civil Society amesema mirathi sio suala la kupasua familia na kusababisha migogoro ni vyema kwa wanafamilia anapokufa mtu kuzingatia ugawaji wa mali kwa njia ya kurithi ili kila mwanafamilia kupata haki yake kisheria na kuepuka migogoro ambayo ni canzo cha uvunjifu wa amani.

.

Asha Suleiman mwanasheria kamesheni ya ardhi amewaasa jamii inapofikia hatua ya kurithi mali zao ni vyema kurithi mapema na kutafuta hati miliki ili zioneshe kama wao ndio wamiliki halali wa ardhi hizo ili kuepusha  migogoro katika familia zao

.

Ali abdalla said na isa nassor, wameiomba serikali kupitia taasisi ya wakfu na mali ya amana kupanua elimu ya mirathihadi vijijini  ili jamii kuweza kuitumia taasisi kupata miongozo ya kurithi sambamba na kujua umuhimu wa mirathi pindi mtu anapofariki ili kudumisha amani visiwani Zanzibar.