Mkoani FM

Kilio  kwa wananchi wa Mjini Kiuyu kutotumika jengo lao la kituo cha Afya

8 September 2023, 9:01 am

Picha ya kituo cha Afya kilichojengwa na wananchi toka mwaka 2011(Picha Fatma Hamad)

Wananchi wa Mjini Kuyu Wilaya ya Wete wakililia miaka 12 tangu kujengwa kituo cha Afya katika kijiji chao kwa lengo la kusaidia kwa mama wajawazito kupata  huduma kwa wakati ila bado seriakali hawajakitumia kituo hicho kama wanavyohitaji wananchi hao.

Na Fatma Hamad.

Wananchi wanaoishi kijiji cha Mjini Kuyu Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba,  wavunja ukimya na kutoa kilio chao  kutokana  baada ya kuwekeza nguvu na pesa zao kwa  ajili ya kujenga kituo cha afya, lakini kimeshindwa kutumika na kutoa huduma kwa sababu ya kukosekana kwa wahudumu wa Afya .

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao Mwananchi  khamis  Omar  ameeleza kuwa walifanya mchango nyumba hadi nyumba  wa vifaa vya ujenzi pamoja na kushiriki katika ujenzi na kujenga kituo cha afya, na   Serikali ikawasaidia  katika kuwezeka kituo hicho. 

 Hata hivyo, tokea mwaka 2011  mpaka sasa kituo  hicho  hakitumiki  na  kimekuwa  gofu.  

Amesema huu ni mwaka wa 12 tokea kujengwa kwa kituo hicho, ambapo kilifunguliwa  na  mbio za mwenge kwa shangwe na nderemo, ili kuondosha shida za wananchi wa kijiji hicho.

 Ameeleza baada ya kuona wanapata tabu kwa kufuata huduma za afya masafa marefu, ndipo wakamua wao wenyewe  kujitolea kujenga ili waondokana na kadhya hiyo, lakini  bado wanaendelea tu kuteseka.

Mapema mwanachi  Raya  Hassan  Amesema kukosekana kwa kituo cha afya karibu na makaazi yao wanapata shida hususan wanapopata mgonjwa wakati wa usiku.

Ameeleza  wanachukua  masafa  kilo mita nne kufuata huduma ya afya, ambapo  wanalazimika kupita sehemu za vichaka na mabonde.

Aidha   ameeleza  kuwa kukosekana kwa kituo cha afya kunachangia  kwa kiasi kikubwa  wa mama wajawazito   kujifungulia majumbani.

Amesema kuwa uzazi wa sikuhizi ni mashaka, hivyo ni vyema kituo kiweze kutoa huduma ili kulinda usalama wa mama na mtoto.

Diwani wa wadi  hiyo Bi Nasra  amesema yeye pamoja na sheha tayari wameshafuatilia kila sehemu ili kuona kituo hicho kinatoa huduma, lakini imeshindikana.

Afisa mdhamini wizara ya Jinsia  na maendeleo ya jamii Khamis Bilal Ali  alifahamisha kuwa wanajenga Hospitali  katika eneo la kiuyu minungwini ambayo itawanufaisha wananchi wa Minungwini pamoja na wa  mjini kuyu.

Amesema kuwa  jingo hilo walilolijenga watalitumia kukiwa na kesi maalumu kama vile mripuko wa maradhi pamoja na kipindi cha utoaji wa chanjo za watoto.