mwananchi akiiyomba serekali kutoa elimu ya corona
Mkoani FM

Wananchi Pemba waomba Elimu ya Uviko-19

28 September 2021, 11:18 am

Mwananchi aiomba serekali kutoa elimu kuhusu corona

Na Fatma Suleiman

Wananchi kisiwani pemba wameiomba serikali kutoa elimu kuhusu korona wimbi la tatu, ili kuongeza uelewa  na kuzidisha tahadhari  ya kujikinga na maambukizi hayo kwa wanajamii

Wakizungumza na habari hizi baadi ya wananchi hao, wameeleza kuwa awali ilipoingia korona serikali ilikuwa inatoa tahadhari na elimu kwa  hali ya juu tofauti na sasa  jambo ambalo linasababisha  wananchi kupunguza hali ya tahadhari kwa ugonjwa huo.

Aidha wameeleza kuwa bado jamii imekosa uelewa juu ya upatikanaji wa chanjo dhidi ya uviko 19 jambo ambalo linapelekea wananchi wa kawaida kutopiga chanjo hiyo.

Meatibu kitengo cha elimu ya afya pemba aAbeid Ali Ali amesema kuwa  kitengo hicho kinatoa elimu   katika maeneo mbali mbali licha ya uelewa wa wanajamii

Katika kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo kwa wananchi  ni vyema serikali ikaendelea kupaza sauti kwa wananchi  ili kuchukua tahadhari zaid.