Mkoani FM

Waandishi  wa habari Pemba  kupewa mbinu mpya kuandika habari za udhalilishaji

26 August 2023, 8:53 am

Waandishi wa habari wakipatiwa mafunzo katika ofisi za Tamwa Pemba(Picha Khadija Ali)

Waandishi  wa habari Kisiwani Pemba  kupatiwa mafunzo maalum ya uandishi wa  habari za udhalilishaji kwa lengo la kuisaidia jamii endapo  watapata kadhia hiyo.

Na Khadia Ali

Waaandishi wa habari kisiwani Pemba wametakiwa kufanya ufuatiliaji wa  kuzielezea na kuzichakata kwa kutumia takwimu habari zinazohusu masuala ya udhalilishaji wa kijinsia Ili kuleta mabadiliko katika jamii.

Wito huo umetolewa na Afisa Mkuu wa Mawasiliano kutoka TAMWA – ZANZIBAR Safia Ngalapi wakati akifungua mafunzo ya siku tatu yanayohusu uandishi wa habari za udhalilishaji amesema lengo nikuwakumbusha kuendelea kuandika habari hizo  ili kuisaidia jamii.

Afisa Mkuu wa Mawasiliano kutoka Tamwa – Zanzibar Safia Ngalapi

Amesema jamii inauwelewa mdogo kuhusu dhana ya udhalilishaji na ndio mana matendo hayo yanaongezrka  siku hadi siku.

Amesema utafiti uliofanywa na Shirika la Elimuna Sayansi na Utamaduni UNESCO kwa kusirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzani – Zanzibar katika kipindi cha mwezi January –March kwa baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo magazeti,radio na mitandao ya kijamii Bado haijawafikia walengwa jambo ambalo linapelekea kukithiri Kwa vitendo hivyo.

Akiwasilisha mada ya majukumu ya waandishi wa habari mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA Aiman Duwe amesema ni kuchunguza kwa undani habari zinazohusu udhalilishaji sambamba na kuwataka kuwa na moyo wa kujitolea ili lengo la mafunzo hayoliweze kufikiwa.

mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA, Aiman Duwe

Nae mkufunzi Ali Mbarouk Omar akiwasilisha mada ya Uandishi wa habari za uchunguzi amewataka waandishi hao kujenga uthubutu wakati wanapotekeleza majukumu yao kwa kuandika habari zenye ushahidi na kusoma nyaraka mbali mbali ili kuandika habari zenye kuleta tija na mabadiliko kwa jamii.

Jumla ya waandishi 15 kisiwani pemba wamepatiwa mafunzo ya namna ya kuripoti habari zinazohisu udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto.