Mkoani FM

ZALHO kutoa msaada bure wa kisheria kwa wanzanizbari

17 August 2023, 10:50 am

Kulia ni Mratibu wa ZALHO Siti Habibu na kushoto mwanasheria wa shirika hilo Khalfani Amour wakitambusha shirika lao na kutaja malengo yao kwa wananchi .(Picha Khadija Ali)

Shirikala msaada wa kisheria na haki za binaadamu Zanzibar likielezea malengo yake ya kuwasaidia wananchi wanyonge Zanzibar ili waweze kupata haki zao za kisheria hasa kwa wale ambao watashindwa kuwa na mawakili wa kuwasaidia wanapohitaji msaada wa kisheria.

Na Fatma Rashid-Pemba.

Jamii kisiwani Pemba imetakiwa kulitumia Shirikala msaada wa kisheria na haki za binaadamu Zanzibar  ili kusaidiwa changamoto za kisheria zinazowakabili.

 Ameyasema hayo mratibu kutoka shirika hilo Siti Habibu Mohd wakati akizungumza katika kipindi cha ijuwe  sharia kinachorushwa redio jamii mkoani katika harakati za kulitangaza shirika la msaada wa kisheria na haki za binaadamu Zanzibar ndani ya  Wilaya ya Mkoani.

Amesema lengo la kuazishwa shirika hilo ni kutokana na  uhitaji  wa wanajamii hususani wanawake watoto, vijana na watu wenye ulemavu kutokuwa na uwezo wa kuwakodi wanasheria wanapofikwa na changamoto zinazo hitaji msaada wa kisheria .

Kwa upande wake mwanasheria Khalfan Amour Mohd ameelezea baadhi ya kazi wanazozifanya zikiwemo kutoa msaada wa kisheria katika masuala  ya ardhi,deni ,mikataba,na masuala yanayohusiana na haki za binaadamu pamoja na kutoa elimu kwa wanajamii juu ya utaratibu wa kisheria.

Amefafanua kuwa huduma zote zinazotelewa na shirika hilo ni bure hazihitaji gharama yoyote na hata kwa upande wa mtu mwenye uwezo wa kukodi mwanasheria anaweza kufika katika shirika lao na kupatiwa ushauri utakao msadia katika kupata haki yake.

Shirika la msaada wa kisheria na haki za binaadamu Zanzibar  limeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia wanajamii kutatua changamoto za kisheria na kutetea haki za binaadamu kwa wananchi na kwa upande wa Pemba ofisi zao zipo Mkanjuni chakechake Pemba.