Mkoani FM

Redio za kijamii Zanzibar kupelekwa kidijitali

9 August 2023, 8:32 am

Mkufunzi kutoka TADIO Hilali Ruhundwa akitoa mafunzo ya Redio Portal kwa waandishi wa habari wa Redio za kijamii Zanzibar ( Picha Na Said Omar).

Radio za kijamii Zanzibar wamepatiwa mafunzo maalum ya kuweka habari na vipindi kwenye mtandao (Radio Portal) ili kusomwa na kusikika duniani kote.

Waandishi wa habari redio za kijamii wametakiwa kutumia mtandao ili kukuza taaluma na kuongeza wasomaji na wasikilizaji.

Wito huo umetolewa na mkufunzi kutoka mtandao wa Radio za Kijamii Tanzania TADIO Hilali Ruhundwa wakati akitoa mafunzi ya namna ya kuweka habari katika mtadao katika ukumbi wa Kariakoo mjini Unguja.

Amesema kuwa na utaratibu wa kuweka habari katika mtandao huo kunasaidia waandishi na chombo cha habari kujenga uwelewa na kuwepo katika soko la ushindani kitaaluma.

Akieleza lengo la mafunzo hayo afisa usimamizi kutoka TADIO Fatma Ali amesema ni kuviwezesha vyombo vya habari kuweza kutuma habari zao katika mdandao wa radio portal ili kwenda sambamba na kasi ya ushindani wa kihabari ulimwenguni.

Sauti ya Fatma Ali kutoka TADIO

Ali Khamis moja ya washiriki wa mafunzo hayo wameushukuru mtandao wa radio za kijamii Tanzania TADIO kwa kuwapatia mafunzo hayo na kusema kuwa watayafanyia kazi mafunzo hayo ili yalete faida kwenye  vitio vyao.

Sauti ya Ali Khamis

Mafunzo hayo ya siku mbili yenye lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya kijamii  vya Zanzibar yalifanyika katika ukumbi wa Kariakoo  Unguja.