Mkoani FM

Wahandisi watakiwa kusimamia wakandarasi miradi ya maji Pemba 

3 October 2023, 10:55 am

Kukamilika kwa  miradi ya maji safi kisiwani Pemba yanayotarajia kufikia kila kijiji baada ya kukamilika  miradi hiyo  itafika kila  kijiji na kuwafikia wananchi kwa masaa 24 bila ya kukatika.

Na fatma Rashid

Msimamizi wa huduma za jamii kutoka Ofisi ya Raisi Ikulu Taasisi ya Usimamizi na Ufuatiliaji Utekelezaji Serikalini  Dr. Ibrahim Kabole amewataka wahandisi wa mradi wa maji kuwasimamia wakandarasi ili kuhakikisha wanakamilisha kazi kwa muda uliopangwa.

Ameyasema hayo katika ziara yake mkoa wa Kusini Pemba wakati akikagua matenki ya maji yaliyojengwa kupitia fedha za ahueni ya uviko 19 yaliyopo kijiji cha Kendwa, Pujin na Chanjaani.

Mwenyekiti wa taasisi ya  WASH  Francis Odhiambo  amesema taasisi yao itaendelea kutoa  msaada ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar  ZAWA  Dkt. Salha Mohd Kassim amesema kukamilika kwa mradio huo utasaidia  upatikanaji wa maji  safi na salama  kwa masaa 24, kulinganisha na hapo awali.

Vilevile Mkuu wa Mawasiliano na Habari kutoka PDB  Mohd Mansour ameitaka Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar  kuendelea kushirikiana vyema na ZAWA pamoja na wadau wengine ili kuunga mkono maendeleo yanayoletwa na serikali katika sekta ya maji na zingine ili kufikia malengo yaliyowekwa.

Ziara hiyo  imeandaliwa na PDB Ofisi ya Rais Ikulu Taasisi ya Usimamizi na Ufuatiliaji Utendaji Serikalini ikishirikiana na ZAWA ambapo waliambatana na wadau wengine wa maji  kwa lengo la kuangalia ukamilishwaji wa miradi ya maji ya ahueni  ya Uviko19 katika mkoa wa Kusini Pemba.