Mkoani FM

Dkt. Khalidi: Tusichafue bahari kwani asilimia 50 ya oxygen inatoka huko

29 September 2023, 4:37 pm

Waziri wa ujenzi mawasoliano na uchukuzi Zanzibar Dr Khalid Salim Ali(Picha Fatma Rashid)

Wananchi waache kuchafua mazingira ya bahari ili ibaki katika haiba yake na kuwalinda viumbe hai wanaopatikana ndani yake.

Na fatma Rashid.

Waziri wa Ujenzi, Mawasoliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt. Khalid Salim Ali ameitaka jamii kuacha tabia ya kutupa taka  ovyo baharini na ukataji wa mikoko Ili kulinda mazingira safi ya bahari.

KAULI hiyo ameitoa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya bahari Dunia  yaliyofanyika katika viwanja vya Gombani  Chake chake Pemba amesema  asilimia kubwa ya watu na viumbe vya baharini wanategemea oxygen ambayo kwa asilimia 50 inatokana na bahari hivyo ni vyema kuyatunza Ili kuendeleza Haiba ya bahari iliyopo.

Pia amesema kuwa licha ya kuwepo kwa  bahari lakini bado  kuna baadhi ya watu hawatambui umuhimu wa uwepo wa bahari, hivyo amewataka wananchi kuchukua hatua za makusudi  kulinda na kuhifazi mazingira ya baharini.

Kwa upande wake Mkurugenzi i wa mamlaka ya usafiri majini ZMA Shekha  Ahmed Mohd  amesema wananchi kupitia wizara ya  Uchumi wa buluu wamejikita katika shuhuli mbali mbali zikiwemo kilimo cha  mwani , uvuvi ,utalii ,ufugaji wa majongoo utafutaji wa mafuta na shuhuli nyengine za kujipatia ziski ,hivyo amewataka wananchi kutunza mazingira na kufuata sheria ili kujikinga na madhara yanayoweza kujitokeza.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba salama Mbarouk Khatib ameishukuru serekali ya Tanzania bara SMT  kwa kushirikiana na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar SMZ  katika kufanikisha jambo hili . 

Aidha Mkurugeni wa Usalama wa Mazingira ,Wizara ya Uchukuzi Tanzania Stella Joshua Katondo  amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuibua uelewa kwa watu juu ya utunzaji wa mazingira ya bahari pamoja na fursa zinazopatikana kwenye bahari. 

Maadhimishi ya siku ya bahari duniani hifanyika Kila September 28 ya Kila mwaka na mwaka huu yamefanyoka ktk viwanja vya gombani chake chake Pemba na kauli mbiu ni Miaka 50 ya marpol uwajibikaji wetu unaendelea.