Mkoani FM

Kampuni ya  MECCO yapewa mwezi mmoja kukamilisha vifaa vya ujenzi wa barabara Pemba

30 September 2023, 6:03 pm

Waziri wa ujenzi mawasiliano na uchukuzi Dr khalid Salum Mohd (Picha Fatma Rashid)

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haijaridhishwa na utengenezaji wa mradi wa barabara ya Chakechake – Wete, ambayo imeshatumia miezi 19 tangu ilipoanza kutengenezwa.

Na fatma Rashid

Waziri wa ujenzi mawasiliano na uchukuzi Dkt. Khalid Salum Mohd amesema hajaridhishwa na utendaji kazi wa kampuni ya   MECCO inayojenga barabara ya chake chake – wete .

Ameyasema hayo wakati wa ziara ya kutembelea barabara hiyo kwa lengo la kutaka kujua maendeleo yaliyofikiwa na kukuta hali isiyoridhisha kulinganisha na muda uliotokewa na hatua iliyofikiwa .

Hivyo amewatalka wakandarasi kuchukua hatua za kutatua changamoto zilizopo ndani ya mwezi mmoja kwa lengo la kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ili kuwapunguzia kadhia ya vumbi wakaazi wa maeneo hayo linalotokana na kifusi cha barabra hiyo.

Kwa upande wake  Mhandisi Mkaazi Adam Makoba amesema hali ya uendeshaji na utekelezaji wa barabara hiyo bado unasuasua na maendeleo yaliyopo ni madogo sana kutokana na ukosefu wa baadhi ya vifaa vya kutendea kazi.

Meneja Mradi Charles Mwengende amesema kusua sua kwa mradi wa ujenzi wa barabara hiyo kunasababishwa na changamoto ya majengo yaliyopo katika maeneo ya mradi huo.

Nae mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba Salama  Mbarouk Khatib amsesema serekali itakuwa bega kwa bega kutoa masjhirikiano hivyo amewataka wakandarasi Kutoa taarifa endapo kutakuwa na watu waliogoma kupisha ujezni wa barabara hiyo huku wakiwa wameshapewa fidia  ya majengo yao na watachukuliwa hatua .

Ziara hiyo ni ya ufuatiliaji wa maendeleo ya miradi ya barabara iliyoanza kufanyiwa kazi na kampuni zilizoingia ubia na serekali  ya mapinduzi ya zanzibar kujenga barabara za kisasa katika mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo barabara ya cheke Wete inajengwa na Cammpuni ya MECCO