Mkoani FM

TAMWA Zanzibar: waandishi wa habari wanolewa kuwasaidia wanawake kuwa viongozi

10 September 2022, 10:46 am

 

Dr. MZUR ISSA MKURUGENZI WA CHAMA CHA WAANDSHI WA HABARI WANAWAKE TANZANIA -ZANZIBAR.

Uwepo wa asilimia ndogo ya ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi ni changamoto moja wapo inayopelekea kutopatikana kwa maendeleo kwa baadhi ya taasisi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa chama cha Waandishi wa Habari wanawake  Tanzania – Zanzibar Dr Mzuri Issa  wakati akifungua mafunzo ya siku 5 ya kuwajengea uwezo waandiahi wa habari  vijana huko katika ukumbi wa afisi hiyo tunguu wilaya ya Kusini Unguja.

Amesema bado hali ya ushiriki wa wanawake kwenye ngazi za maamuzi hauridhishi jambo lililochangiwa mitazamo potofu kwa baadhi ya wanajamii, hivyo ni vyema kwa waandishi wa habari wawe na muono wa mbali katika kusaidia jamii lengo kua na akiba mzuri itakayoleta mabadiliko ya kimaendeleo kwa jamii na taifa kiujumla.

Dr. Ananilea Nkya mkufunzi katika mafunzo hayo amesema kiongozi anaeweza kujitolea ni rasilimali muhimu hivyo ni muda sasa kwa waandiahi kujitoa kuandika habari zitakazoonesha mwanga na kuongeza hamasa kwa wanawake kushinda wakati wanapojitolea kugombania nafasi mbalimbali.

WAANDISHI WA HABAIRI WAKIWA KWENYE MAFUNZO

Ahmed Iddi Haji na Amina Omar  wamesema matarajio ya mafunzo hayo ni kwenda kuengeza uwelewa  kwa wanawake kushiriki  katika ngazi za maamuzi sambaba na kuahidi  kuyafanyia kazi kwa vitendo ili kuleta ufanisi wa kimaendeleo na kufanikisha lengo lamafunzo hayo.

Mafunzo hayo ya siku tano   yenye lengo la kuwajengea uwezo kuandika na kuchambua  habari  zinazohusu wanawake na uongozi  kwa waandishi wa habari vijana  18 kutoka  vyomba mbali mbali vya habari Zanzibar yaliyoandaliwa  na Tamwa Zanzibar  kwa Ufadhili  wa National Endowment for Democracy kutoka Marekani yamefanyika  katika  ukumbi wa Tamwa Zanzibar Tunguu.