Mkoani FM

Walimu watakiwa kuwa wabunifu kuongeza ufaulu.

3 February 2022, 10:52 am

Walimu wa skuli za msingi na sekondari wilaya ya Mkoani wametakiwa kuwa na ubunifu katika ufundishaji ili kuongeza ufaulu kawenye mitihani yao.

Akizungumza mkuu wa wilaya ya mkoani Khatib Juma Mjaja katika kikao cha mikakati ya kujadili tathmini ya matokeo ya kidato cha nne wilaya ya mkoani kilichofanyika katika ukumbi wa wilayani amesema, kutokana na ufaulu ulioipata wilaya ya mkoani ni muhimu kuwa waadilifu katika utekelezaji wa majukumu ya ili kupata matokeo mazuri.

Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Mkoani Bashir Ali Bashir, na DSO Wilaya wamesema ipo haja kwa waalimu wakuu na waalimu wa madarasa kuandaa mazingira mazuri ya ufundishwaji ikiwa ni pamoja na kumaliza mada kwa wakati, kufanya hivyo kutawasaidia wanafunzi kuwa na matayarisho mazuri ya mitihani yao.

Wakati huo huo wamemtaka afisa elimu wilaya kusimamia mipango mikakakati ya walimu wanayoiwasilisha Ofisini kwake kwa vitendo ili kuweka uwiyano sawa katika ufaulu.

Kwa upande wa waalimu waliopata fursa ya kushiriki kikao hicho wamesema sekta ya elimu inakumbana na changamoto nyingi ikiwemo sera, mitaala kutoendana na vitabu vya kufundishia hali inayowapa ugumu katika ufundishaji.

Walimu washiriki wa mkutano

Akitoa ufafanuzi wa hoja zilizowailishwa na washiriki tofauti afisa elimu wilaya ya mkoani Salum sheikhan amesema wizara inafahamu baadhi ya changamoto na zimeanza kufanyiwa kazi hususan sera ya elimu, kwa kuthibitisha hilo ni kureshwa kwa darasa la saba.

Jumla ya wanafunzi 1987 wamesajiliwa Wilaya ya Mkoani wakiwa wanawake ni 1143, wanaume 844 na waliofaulu kwa ujumla wao ni 1096 sawa na asilimia 56.34, kwa kiwango cha ufaulu wa grade 1, 2, 3, na 4.