Mkoani FM

MRATIBU TAMWA:WANAWKE CHACHU YA MAENDELEO WANPOSHIKA NAFASI ZA UONGOZI.

17 March 2023, 1:48 pm

Na Khadija Rashid Nassor.

Uwepo wa viongozi bora na imra Wilaya ya Micheweni na Jimbo la Konde Mkoa wa Kaskazini pemba ni miongoni mwa matunda ya mwanaharakati mwanamke Fathiya Mussa Saidi ambae kwa sasa ni Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari  wanawake Tanzania (TAMWA) Afisi ya Pemba.

Akizungumza na mwndishi wa habari hizi mwanaharakati huyo amesema, ameanza harakati hizi tangua akiwa skuli kwenye ngazi za msingi na  sekondari hadi  kufikia Chuo Kikuu, na kufanikiwa  kua Waziri wa wanawake Chuo cha Ualimu Mkuruma.

Mratibu Fathiya ameongeza kua, cheo cha Uratibu wa TAMWA umemuongezea nguvu za kufanya uhamasishaji na ushawishi sambamba na  kuwajengea uwezo wanawake tofauti ambao kati yao wameshinda changuzi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanwake wanaoshikilia nafasi za uongozi kupiti juhudi za Mratibu Fathiya Mwakilishi wa Jimbo la Konde Zawadi Amour Nassor na Mkuu wa Wilaya ya Micheweni wamesema mafunzo, hamasa smbamba na ushauri walioupata kutoka kwa bi Fathiya Kupitia TAMWA uliwajengea uimara na  kua viongozi.

Omar Mjaka, mmoja wa Wanaume Wakala wa Mabadiliko na Mwanaharakati  Kisiwani Pemba amesema juhudi za Mratibu wa TAMWA ni za kupigiwa mfano kwani amekua akijitolea kuhakikisha wanawake wanapata elimu ya utetezi sambamba na kushiriki kwenye ngazi za maamuzi.

Wakati huhohuo huhamasish wanaume kuachana na mifumo dume na kuwataka kuunga mkono ndoto za wanawake kushiriki kwenye Demokrasia Siasa na Uongozi.