Mkoani FM

ZAFELA kuwarudhisha watoto wa kike shule

21 August 2023, 3:20 pm

Mkurugenzi wa chama cha Wanasheria wanawake Zanzibar ZAFELA Jamila Mahmud(Mwandishi wetu)

Jumuiya ya wanasheria wanawake Zanzibar yapania kuwarejesha skuli  watoto wa kike waliokatisha  skuli wakiwa  bado hawajafikia umri wa kumaliza kwa kushirikiana na taasisi za serikali na NGOs.

Na Fatma Hamad

Asasi za kiraia zimetakiwa kushirikiana kwa pamoja katika kuwajengea uwezo Watoto wa kike,  walioacha Skuli  ili kuendelea na masomo.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa chama cha Wanasheria wanawake Zanzibar ZAFELA Jamila Mahmud wakati akiutambulisha mradi wa Malala, utakaoendeshwa na Zafela visiwani Zanzibar  kwa muda wa mwaka mmoja.

Amesema kwa mujibu wa utafiti walioufanya  waligundua kuna  wimbi la watoto wa kike  waliokatisha masomo yao kutokana na kuolewa, mimba za utotoni pamoja na kufanyishwa  kazi za nyumbani.

Sauti mkurugenzi ZAFELA

Mapema msimamizi wa mradi Hairun Abass Rajab kutoka  chama cha wanasheria  wanawake Zanzibar [Zafela] ameeleza kuwa hadi sasa bado zipo familia ambazo hazimpi fursa mtoto wa kike kupata haki yake ya elimu kuanzia Msingi hadi Vyuo vikuu.

Mwanaharakati wa kulinda na kutetea  haki za wanawake na Watoto kutoka Wilaya ya Mkoani  Sada Moh’d Othman amesema ni vyema kuweko na mkakati Madhubuti ya usimamizi   wanafunzi hao na tusichukulie kuwa umaskini ni sababu ya kutowasomesha watoto wakike.

Sauti mwanaharakati

Mradi  huo wa mwaka mmoja umelenga kuwafikia jumla ya watoto  3,000 kwa  Unguja na Pemba wenye lengo wa kuwarudisha watoto wakike skuli.