Mkoani FM

Tasisi ya TAMWA na TUJIPE wapania kumaliza suala la udhalilishaji

22 February 2023, 11:26 am

NA Amina Masoud

WAZAZI na walezi kisiwani Pemba wamezishukuru taasisi za kiharakati zinazo ongozwa na wanawake kwa kuwapatia elimu ya kutoa ushahidi Mahakamani ili kuepuka kumaliza kesi za udhalilishaji katika ngazi za familia.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wazazi wa wahanga wa udhalilishaji Amina Ali Hasaan na Haji Juma Kheir majina yao sio halisi wamesema, elimu waliopatiwa kupitia viongozi kutoka Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar Ofisi za Pemba na Jumuiya ya Tumaini Jipya Pemba TUJIPE imewasadia kupata uwelewa na kutoa ushahidi mahakamani hali iliyochangia kuwashawishi kwenda kutoa ushahidi mahakamani kila wanapohitajika.

Wazazi

Mratibu wa TAMWA Pemba Fathiya Musa Said na Mkurugenzi wa TUJIPE  Tatu Abdallah Mselem wamesema hatua hiyo imekuja kutokana na watu wengi hususani akina mama kukosa haki zao stahiki na watoto kudumaa kwa ndoto zao za kuwa viongozi kwa kufanyiwa ukatili wa kingono na kukosa haki zao.

Mratibu wa wanawake na watoto shehiya ya Msingini Tamim Kharoun Rashid ameziomba taasisi nyengine na mashirika binafsi kuiga mfano wa taasisi ya TAMWA na TUJIPE kwani elimu wanayoitoa imesaidia kupunguza kesi ya matendo hayo katika shehiya yake.

Fathiya Musa Said, Mratibu wa TAMWA Pemba na   Tatu Abdallah Mselem,Mkurugenzi wa TUJIPE.

Nae Seif Mohd Khamis wakili wa serikali dhamana   Mkoa wa Kusini ambae pia ni Kaimu Mwanasheria Dhamana Pemba amesema kutokana na miongozo ya ofisi hiyo jalada huchukua masaa 24 kuwepo hapo na endapo ushahidi hauna changamoto linaweza kufanyiwa maamuzi ya haraka sambamba na kuiangalia jamii kuwa na hamu ya kutoa ushahidi na hii inatokana na elimu wanayopatiwa na viongozi hao kuhusu matendo hayo.

Nd,Seif Mohd Khamis wakili wa serikali dhamana   Mkoa wa Kusini

Hakimu wa mahakama maalum ya kusikiliza kesi za udhalilishaji Muumini Ali Juma amesema hatua zilizochukuliwa na taasisi hizo chini ya viongozi wanawake ni za kupigiwa mfano kwani jamii imepata muamko juu ya kuripoti na kutoa ushahidi mahakamini tofauti na hapo kabla kwani walikuwa wakizimalizia majumbani.

Makosa ya udhalilishaji  yamepungua kutoka kesi 65 kwa mwaka 2021, hadi 44 kwa   mwaka 2022 kuanzia January hadi November  ambapo mashauri 39 yamemalizika na mashauri 5 yanaendelea mahakamani.

MWISHO