Mkoani FM

Wahudumu wa afya wa kujitolea Pemba kuongeza uhamasishaji wa chanjo ya Uviko-19

25 July 2022, 9:35 am

WAHUDUMU WA AFYA WA KUJITOLEA PEMBA  KUONGEZA UHAMASISHAJI WA CHANJO YA CORONA

Mratibu wa kitengo cha chanjo Pemba Bakar Hamad Bakar Pemba

MRATIBU WA KITENGO CHA CHANJO PEMBA BAKAR HAMAD BAKAR

 

Wahudumu wa afya wa kujitolea(CHV) kisiwani pemba wametakiwa kuendelea kuhamasisha jamii kujitokeza kuchanja chanjo ya corona ili kuongeza nguvu ya mapambano dhidi ya UVIKO 19.

Kauli hiyo imetolewa na mratibu wa kitengo cha chanjo pemba bakar hamad bakar wakati akizungumza na wahudumu jamii vinara kwa Wilaya ya mkoani na micheweni.

Ameeleza wizara kupitia kitengo cha chanjo wameweza kuongeza vituo vya uchanjaji lengo ni kuifikia jamii yote hivyo ni jukumu la wahudumu hao sasa kushuka kwa jamii kuendelea kuhamasisha zaid kwani hii ni awamu ya nne ni vyema kujitahidi kufikia lengo husika.

WAHUDUMU WA AFYA WA KUJITOLEA KISIWANI PEMBA

Mapema akifungua kikao cha siku moja cha utambulisho wa mradi kuwajengea uwezo CHV juu ya uhamasishaji jamii kujitokeza kuchanja chanjo ya corona, kaimu afisa mdhamini wizara ya afya yussuf hamad iddi amesema, CHV ni wadau wakubwa hivyo ni muhimu kujitoa na kuifikia jamii ili kuongeza  asilimia kwani idadi ya waliochanjwa bado ni ndogo hali inayoashiria hatari ya kurudi tena kwa UVIKO 19 nchini.

 

Dr. Vedat muwakilishi wa WHO akieleza lengo kuu la mradi amesema ni kufikia hali ya juu ya uchanjaji, aidha ameiasa jamii kujitokeza kuchanja kwani kurudi tena kwa ugonjwa huu kutasababisha gharama makubwa kwa watu na itapelekea kushuka uchumu wa serikali na kusimama ashughuli nyingi za  kiuchumi na kupelekea kuongezeka  gharama za Maisha.

CHV wa wilaya zote  mbili (2) waliopata fursa katika mradi huo wameahidi kuendelea kuyafanyia kazi kwa vitendo yale yote waliyoelezwa lengo ni kufikia asilimia 80 ya uchanjaji ikiwa ni hatua moja wapo ya kuukimbiza kabisa ugonjwa huu.