Mkoani FM

Usafiri wa haraka kikwazo kwa mama na mtoto kupata humduma za afya Pemba

27 October 2023, 7:29 pm

Mkuu wa kituo cha Afya Wesha AbdulNasir Hemed Said(Picha Khadija Ali)

Huduma za mama na mtoto bado ni changamoto kwa baaddi ya vijiji kisiwani Pemba kwa kukosa usafiri wa haraka wanapohitaji kuelekea kituo cha afya kwa ajili ya kupata huduma za afya.

Na Khadija Ali

WAUGUZI wanaotoa huduma za Mama na Mtoto wamesema licha ya kuanzishwa kwa mfumo wa M mama lakini bado  lengo la kutoa usafiri wa haraka wakati ikitokezea tatizo kwa kundi hilo hauja fanikiwa ipasavyo katika vituo hivyo.

Wakizungumza na wandishi wa habari hizi Amina Ali Abdi muuguzi mkunga kutoka kituo cha Afya Wesha na Muuguzi Mkunga kutoka kituo cha Afya Pujini Nasra Abdalla Juma wamesema inapotokezea tatizo la mama na mtoto huduma hiyo inakua changamoto ya  usafiri wa kuwapehisha katika Hospitali za rufaa  jambo linalohatarisha maisha kwa wazazi.

Kwa upande wake Mkuu wa kituo cha Afya Wesha AbdulNasir Hemed Said amesema ili kufikia lengo la mfumo wa M mama kama ilivyotarajiwa, ameiomba Serikali kuboresha huduma hiyo na kunaondosha vifo vya mama na mtoto kama ilivyo dhamira ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

Afisa Mdhamini Wiraza ya Afya Pemba Khamis Bilali Ali amesema Wizara imeweka mpango mkakati wa kuongeza madereva wa Ambulesi ambao watafanya kazi usiku na mchana katika kuwafikisha wagonjwa Hospitali kupata huduma kwa wakati.

Mratibu wa huduma ya mfumo wa M mama Ofisi ya Pemba Maryam Ali Said amesema wameshaweka mpango wa kuhakikisha madereva wote waliosajiliwa na wizara wanapata malipo yao kwa wakati ili kuona wanafanya kazi masaa 24 na kwa bidii.

Sera ya Wizara ya Afya ya Zanzibar ya mwaka 1990 ni kuhakikisha inaimarisha huduma za Afya ya uzazi kwa mama na mtoto, ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi  na vya watoto wachanga.