Mkoani FM

Waziri Mbarawa akabidhi vifaa vya ujenzi wa skuli vyenye thamani ya milioni 50

9 September 2023, 2:28 pm

Katibu wa mbunge  wa jimbo la Mkoani Mariam Said Khamis akizungumza na wananchi wa shehia ya chokocho wakati akikabidhi vifaa vya ujenzi vya skuli.

Prf,  Mnyaa Mbarawa akitekeleza ahadi yake ya kuwajengea skuli  wananchi wa sheia ya Chokocho ambapo  kwa sasa eneo hilo kuna skuli moja tu ambayo wanasoma wanafunzi wa sekondari na  Msingi wakiingia kwa nyakati za asubuhi na mchana .

Na Khatib Nahoda.

Jumla ya shilingi Milioni 50 zinatarajiwa kutumika katika hatua ya mwanzo ya ujenzi wa mabanda ya kusomea ya skuli ya chokocho wilaya ya mkoani mkoa wa kusini Pemba.

Akizungumza mara maada ya kukabidhi vifaa  vya ujezi wa mabanda nane kwa kamati ya skuli hio katibu wa mbunge  wa jimbo  mkoani Mariam Said Khamis kwa niaba ya Mbunge wa jimbo hilo Profesa Makame Mbarawa amewataka  wanachi wa wajimbo hilo kuunga mkoano juhudi za kimaendeleo zinazo fanywa na mbunge wao kwa lengo kuleta maendeleo.

Wananchi wa shehia ya chokocho jimbo la Mkoani Pemba

Amesema kwa niabaya mbunge huyo ata hakikisha ujenzi huo uliopo hatua ya awali unakamilika na hatua ya pili ili kuondosha changamoto ya uhaba wa vyumba vya kusomea.

Sambamba na hayo amewataka wananchi wa shehia hio ya chokocho kutoa ushirikiano kwa amafundi na kuhakikisha wanakua walinzi wa vifaa vilivyotolewa ili lengo la ujenzi  litimie kama ilivyokusudiwa.

katibu wa mbunge  wa jimbo la  mkoani Mariam Said Khamis

Nae mwenye kiti wa CCM jimbo la mkoani Omar Ngwali Dadi amesema kutolewa kwa vifaa hivyo ni utekelezaji wa ilani ya chama na utekelezaji wa ahadi alizoziweka mbunge huyo.

Idi Abdala Idi mwenye kiti wa kamati ya  skuli ya chokocho sekondari amesema mabanda hayo yatakapo kamilika yataondosha changamoto  walioyonayo kwa muda mrefu pia ufaulu wanafunzi utaongezeka.

Idi Abdala Idi mwenye kiti wa kamati ya  skuli

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa  skuli ya sekondari chokocho Haji Shoka amesema ujenzi huo wenye vyumba nane vya kusomea , maabara, chumba cha komputa, ofisi za walimu pamoja na vyoo utakapo kamilika utatoa ufanisi wa ufundishaji kwa walimu na kuongeza kiwangocha ufaulu.

Amesema kwa sasa skuli hiyo ina mchanganyiko kwa wanafunzi wa sekondari na msingi kwa kuwakosesa wanafunzi utulivu wa kosoma na kupelekea matokeo yao kutokua mazuri kama inavyotarajiwa.

Mwalimu mkuu wa  skuli ya sekondari chokocho Haji Shoka

Vifaa vilivyo kabidhiwa kwahatua ya awali katika skuli ya chokocho ni mawe, matofali,kokoto , nondo, mchanga pamoja na suruji pakti 300.