Mkoani FM

DC Miza aibeba Kiwani Combine

20 July 2025, 12:09 pm

Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Miza Hassan Faki akikabidhi mchango wa serikali ya wilaya kwa katibu wa timu ya Kiwani Combine ofisini kwake Mkoani. (Picha na Said Omar)

Mkuu wa Wilaya ya Mkaoni Pemba amekabidhi mchango wa Serikali ya wilya ya Mkoani ikiwa ni kuiunga mkono timu ya Kiwani Combine inayoshiki mashindani ya Yamle Yamle.

Na Khatib Juma Nahoda

Wadau wa michezo kisiwani Pemba wametakiwa kuiunga mkono timu ya Kiwani Combine ili iweze kufikia lengo la kushiriki mashindano ya Yamle Yamle.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Miza Hassan Faki wakati akikabidhi mchango wa Serikali ya wilaya katika maandalizi ya timu hiyo ofisini kwake Mkoani Wilaya ya Mkoani Pemba.

Amesema serikali ya wilaya imeona ipo haja ya kuiunga Mkoani timu ya Kiwani Combine ili iweze kushiriki, kushinda na kuipa heshima Wilaya ya Mkoani katika sekta ya michezo.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya amesema michezo ni sehemu ya fursa ya kiuchumi kwani vijana huweza kupata nafasi ya kuonekana na timu vyingine kutangaza vipaji vyao, hivyo amewataka vijana wa timu hiyo kuitumia vyema fursa hiyo ili iweze kuwatangaza maeneo mbalimbali.

Aidha amesema michezo ni zaidi ya burudani kwani huleta umoja na kuimarisha afya bora kwa vijana.

Aidha ametumi fursa hio kuwataka viongozi na wachezaji wa timu hio kwenda kudumisha nidhamu wakati wa mashidani na baada ya mashindi kwa nidhamu ndio kitu pekee kitakacho wezesha kupata zawadi hata kama wakishindwa kufika mbali katika mashindano hayo.

Suleiman Nassor Suleima katibu wa kiwani combain umeushukuru uongozi wa Waliya kupitia Mkuu wa Wilaya ya Mkoani na kumuahidi kufanya vizuri katika mashindani hayo.

Amesea timu hiyo itatoafurasa kwa vijana wa Wilaya ya Mkoani kupata nafasi ya kuonekana na timu nyengine kubwa za Zanzibar na nje ya Zanzibar.

Ali Mbarouk Salum mjumbe wa timu ya kiwani combain amewataka vijana wa wilaya ya mkoani kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu hio kwani ni fursa kwako ya kutambulika kimichezo.

Jumla ya shilingi laki 3 pamoja na kilo 75 za mchele zimetolewa na serekali ya wilaya kwa ajili ya maandalizi ya timu hiyo kuelekea mashindani ya yamle yamle kwa mwaka 2025.