Wananchi Pemba waomba Elimu ya Uviko-19
28 September 2021, 11:18 am
Na Fatma Suleiman
Wananchi kisiwani pemba wameiomba serikali kutoa elimu kuhusu korona wimbi la tatu, ili kuongeza uelewa na kuzidisha tahadhari ya kujikinga na maambukizi hayo kwa wanajamii
Wakizungumza na habari hizi baadi ya wananchi hao, wameeleza kuwa awali ilipoingia korona serikali ilikuwa inatoa tahadhari na elimu kwa hali ya juu tofauti na sasa jambo ambalo linasababisha wananchi kupunguza hali ya tahadhari kwa ugonjwa huo.
Aidha wameeleza kuwa bado jamii imekosa uelewa juu ya upatikanaji wa chanjo dhidi ya uviko 19 jambo ambalo linapelekea wananchi wa kawaida kutopiga chanjo hiyo.
Meatibu kitengo cha elimu ya afya pemba aAbeid Ali Ali amesema kuwa kitengo hicho kinatoa elimu katika maeneo mbali mbali licha ya uelewa wa wanajamii
Katika kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo kwa wananchi ni vyema serikali ikaendelea kupaza sauti kwa wananchi ili kuchukua tahadhari zaid.