Highlands FM
Highlands FM
26 March 2026, 11:33

Usafi wa masikio ni jambo muhimu katika kulinda afya ya binadamu, ingawa unapaswa kufanywa kwa uangalifu ili kuepuka madhara.
Na Mwanaisha Makumbuli.
Usafi wa masikio ni muhimu kwa afya ya binadamu, lakini unapaswa kufanyika kwa uangalifu mkubwa.
Kitaalamu, masikio yana uwezo wa kujisafisha yenyewe kupitia utengenezaji wa nta ambayo husaidia kuzuia vumbi, bakteria na uchafu kuingia ndani ya sikio.
Mwandishi wetu, Mwanaisha Makumbuli, amefanya mahojiano na mtaalamu wa masuala ya masikio na usikivu ZERA KAYANDA kutoka Hospitali ya Kanda Rufaa Mbeya, kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa afya ya masikio.
Katika mahojiano hayo, awali Mwanaisha ameanza kwa kumuuliza swali la msingi kuhusu sikio ni nini?