Highlands FM

Wananchi Wahimizwa Kushirikiana na Dawati la Jinsia Kupinga Ukatili

9 March 2026, 10:24

Afisa Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Iringa Loveness Maingu

Jamii imetakiwa kuendelea kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa mapema kuhusu vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Na Mwanaisha Makumbuli

Afisa Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Iringa Loveness Maingu amesema bado kuna matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto yanayoripotiwa katika mkoa huo, huku akisisitiza umuhimu wa jamii kutoa taarifa mapema ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa wahusika.

Akizungumza katika mahojiano maalum, na Mwanaisha Makumbuli   ambaye ni Mwandishi wa habari amesema kuwa dawati hilo linaendelea kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kuwasaidia waathirika wa ukatili ili kuhakikisha haki zao zinalindwa.

Sauti Mahojiano