Highlands FM

HESLB mguu sawa mwaka wa masomo Novemba 2025

3 October 2025, 12:30

Katibu Mkuu wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt Kenneth Hosea.Picha na Lameck Charles.

Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 900 kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu, vyuo vya kati na Samia Scholarship kwa mwaka wa masomo 2025/2026, ili kuhakikisha wanafunzi wahitaji kutoka familia za kipato cha chini.

Na Lameck Charles.

Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania imedhamiri kuendelea kutoa fedha za mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na Vyuo vya kati hapa nchini  ili waweze kusoma kwa bidii na kufikia ndoto zao kwa mastakabali wa ujenzi wa Taifa.

Hayo yamesemwa na  Dkt Kenneth Hosea kwa niaba ya Katibu Mkuu wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika ufunguzi wa kikao kazi na kati ya Menejiment ya Bodi ya Mikopo na Maafisa Mikopo kutoka Taasisi za Elimu ya Juuu na Vyuo vya katika  kilichofanyika jijini Mbeya

Sauti Kenneth Hosea

Aidha katibu huyo amesema lengo la serikali ni kuhakikisha wanafunzi wanapata  elimu ya juu na hatimae kushiriki katika ujenzi wa taifa wakiwa wataalamu wa fani mbalimbali.

Sauti Kenneth

Kwa upande wake Dkt. Bill Kiwia, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania amesema Bodi ya ikopo imejipanga vizuri kuhakikisha  inatoa mikopo na kuhakikisha mikopo hiyo inarejeshwa huku akitaja mafaniko waliyoyapata

Sauti Bill Kiwia

Bw.CPA  Anthony Ooko, ni Meneja wa Kanda, Ofisi ya Bodi ya mikopo Mbeya amesema ana washukuru Maafisa Mikopo kwa ushrikiako wao huku wakiweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuendana na matumizi ya kidigitali kwa lengo la kuwahudumia wanafunzi kwa haraka zaid.

Sauti Anthony Ooko

Zaidi ya Maafisa Mikopo laki moja na elfu hamsinina wenyeviti wa Bodi,wawakilishi wa tasisi za fedha toka  Tanzania bara na visiwani wamepiga kambi jijini Mbeya katika kikao kazi cha siku mbili kwa lengo la kijiandaa na mwaka wa masomo unaotarajiakuanza mwezi Novemba  Mwaka huu.