Highlands FM
Highlands FM
10 September 2025, 14:10

CHILD SUPPORT TANZANIA kwa kushirikiana na Hakielimu wamekuja na mpango wa elimu jumuishi wenye lengo la kuyatambua makundi mbalimbali wakiwamo watoto wenye ulemavu Mkoani Mbeya.
Na. Isack Mwashiuya
Katika kusaidia kutimiza mpango wa serikali wa kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu unatimia bila kujali hali yake Taasisi isiyo ya kiserikali ya CHILD SUPPORT TANZANIA kwa kushirikiana na Hakielimu wamekuja na mpango mkakati wa elimu jumuishi (NSIE) wenye lengo la kuyatambua makundi mbalimbali wakiwamo watoto wenye ulemavu na changamoto wanazopitia hususani kwenye suala la elimu ili kutengeneza mazingira wezeshi kwao kupata haki yao ya kielimu.
Akizungumza katika semina maalumu iliyowakutanisha makundi mbalimbali ikiwamo shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemevu Tanzania SHIVYAWATA,wazazi, waalimu,wanafunzi na jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia na watoto iliyofanyika katika ukumbi wa BEACO Jijini Mbeya Septemba 09 2025 Mkurugenzi na mwenyekiti wa bodi kutoka Child Support Jameson Kasati amebainisha kazi za taasisi na lengo la kuanzisha mpango huo.
Sajenti CONSOLATA Mng’ong’o afisa wa polisi kitengo cha dawati la jinsia na watoto mkoa wa Mbeya ameiomba jamii Kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuwaibua wazazi ambao bado wanawaficha watoto wenye ulemavu ndani na kuwanyima haki zao ikiwamo kupata elimu.
Kwa upande wake Damas Mwambeje mwenyekiti kamati za kudumu Child support Tanzania amebainisha mwenendo wa mradi huo mpaka sasa.
Baadhi ya wanafunzi ambao wamehudhuria semina hiyo akiwamo Believer Mwaisela na Rehema Said ambao baadhi yao ni wanufaika wa moja kwa moja wa mradi hawakusita kuishukuru Child Support Tanzania huku wakiwasihi wazazi na jamii kutowakatia tama watoto wenye changamoto ya ulemavu.
