Highlands FM

Ngasa: Wananchi Mbeya jihadhari, baridi kali ni hatari kiafya

24 July 2025, 10:53

Hali ya baridi Mbeya.Picha Samweli Mpogole

Kutokana na baridi kali katika baadhi ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini hasa Njombe, Mbeya na Iringa, wananchi wametakiwa kuchukua hatua za kiafya ili kuepuka magonjwa yanayosababishwa na hali hiyo.

Na Samwel Mpogole

Wananchi wa Mkoa wa Mbeya, hususan wazee na watu wenye magonjwa ya kudumu, wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya athari za baridi kali na vumbi vinavyoendelea kushuhudiwa katika kipindi hiki.
Wito huo umetolewa na Daktari Bingwa wa Mifupa na Mfumo wa Fahamu, Dkt. Elizabeth Ngasa, alipokuwa akizungumza na Highlands FM,ambapo ameeleza kuwa hali ya baridi inachochea maumivu ya mifupa, viungo, na inaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa afya ya watu wenye magonjwa kama kisukari, shinikizo la damu na pumu.

Sauti Elizabeth Ngasa

Katika hatua nyingine, Dkt. Elizabeth ameleza kuwa vumbi inaotokana na ukavu wa hali ya hewa na inaweza kusababisha athari hivyo ni vyema jamii ikawa na tahadhali.

Sauti Elizabeth Ngasa Vumbi

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi hasa wazee, wamesema hali ya hewa ya sasa imekuwa changamoto kwao na kwamba wanafanya jitihada kujikinga kwa kutumia mavazi mazito, kunywa vinywaji vya moto na kupunguza shughuli za asubuhi na usiku ambapo baridi huwa kali zaidi.

Sauti Sauti za Wazee