Highlands FM
Highlands FM
3 July 2025, 13:19

MNEC aeleza sababu za kuto chukua fomu ya ubunge Mbeya
Na Samwel Mpogole
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) kutoka Mkoa wa Mbeya, Ndele Mwaselela, amefunguka kuwa hadi sasa hajachukua fomu ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwaselela amesema licha ya kuwepo kwa maneno mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mustakabali wake wa kisiasa, hajafanya maamuzi ya kuwania nafasi yoyote, bali anajikita zaidi katika kutekeleza wajibu wake wa kuhudumia jamii.
Aidha, amesisitiza kuwa ataendelea kusimamia chama chake kwa uaminifu na uadilifu kwa mujibu wa nafasi yake ya MNEC, huku akiwataka wanaCCM kuendeleza mshikamano na kuepuka majungu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi.
Kauli hiyo ya Mwaselela imekuja wakati ambapo baadhi ya wanasiasa wamejitokeza kuchukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi mbalimbali ndani ya CCM ikiwepo Ubunge, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
