Highlands FM
Highlands FM
3 July 2025, 11:51

TCCIA Mkoa wa Mbeya imeanzisha utaratibu mpya kwa wafanyabishara, ujulikanao kama “chai ya asubuhi.
Na Samwel Mpogole
Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoani Mbeya imeanzisha utaratibu mpya wa kijumuisha wafanyabiashara unaojulikana kama “chai ya asubuhi”, ikiwa ni njia ya kuwakutanisha wadau wa biashara kwa mazungumzo, ushauri na kujadiliana changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Mwenyekiti wa Chemba hiyo, Bw, Erick Sichinga, amesema utaratibu huo unalenga kujenga umoja miongoni mwa wafanyabiashara, kukuza mtandao wa kibiashara na kuweka mazingira bora ya majadiliano yasiyo rasmi baina ya sekta binafsi na wadau wa maendeleo.
Nao baadhi ya Wafanyabiashara wameeleza kufurahishwa na mpango huo wakisema unawapa nafasi ya kufahamiana, kujifunza kutoka kwa wenzao na kupata mrejesho wa moja kwa moja kutoka kwa viongozi wa chemba kuhusu masuala muhimu ya kiuchumi.
