Highlands FM
Highlands FM
1 July 2025, 12:51

Baadhi ya wabunge katika maeneo mbalimbali nchini wakirejesha fomu ambapo zoezi hilo linatarajiwa kufungwa kwesho julai 2,2025.
Na Lameck Charles
Mtia nia wa ubunge wa Jimbo la Mbeya mjini (CCM) Patrick Mwalunenge amewakumbusha watia nia wenzake kuachana na uchonganishi ili kuepusha mpasuko ndani ya Chama, badala yake wawaeleze wananchi nini watafanya ikiwa watateuliwa.
Mwalunenge ametoa tahadhari hiyo wakati akirejesha fomu ya kuwania Nafasi ya Ubunge Jimbo la Mbeya mjini fomu hiyo aliyochukuliwa na Makundi ya Wafanyabaishara na Usafirishaji.
Aidha ametoa wito kwa wananchi mkoa wa mbeya kujitokeza kwa wingi na kutia nia ya kuwatumikia wananchi ikiwa bado zoezi la uchukuaji fomu bado halijafungwa.
Katika hatua nyingine Mwalunenge amewashukuru wananchi wa Mbeya kwa mapenzi ya dhati waliyomuonesha huku akiahidi endapo atapata nafasi ya kuwaongoza hatowangusha
kwa Mujibu wa ratiba ya Chama Cha Mapinduzi mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge na udiwani ni Julai 2,2025 saa kumi jioni.
