Highlands FM
Highlands FM
26 June 2025, 12:23

Kwa mujibu wa ripoti hiyo idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya ulimwenguni imeongezeka na kufikia watu milioni 292 mwaka 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 katika kipindi cha miaka 10.
Na Samwel Mpogole
Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Matumizi na Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya kila tarehe 26 Juni, baadhi ya waathirika wa matumizi hayo wameanza kuvunja ukimya, wakieleza madhara waliyopitia na safari yao ya kupona.
Mwandishi wetu Mwanaisha Makumbuli anasimulia taarifa iliyo andaliwa na Samwel Mpogole, juu ya kijana mmoja aliyewahi kuwa mwanafunzi wa udaktari lakini akaacha masomo kutokana na dawa za kulevya.