Highlands FM

Wananchi Mbeya na matarajio ya bajeti ya taifa 2025/2026

13 June 2025, 16:17

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba. Picha Mtandaoni

Wananchi mkoani Mbeya wameleza matarajio waliyonayo sambamba na changamoto walizoziona katika Bajeti kuu ya Taifa 2025/26

Na Samwel Mpogole

Baadhi ya wananchi mkoani Mbeya wamesema wanatarajia Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2025/2026 iwe na tija katika maeneo muhimu ikiwamo kupunguza gharama za maisha, kukuza sekta ya kilimo sambamba na kuongeza upatikanaji wa huduma bora za afya na elimu.

Wakizungumza na Highlands FM kwa nyakati tofauti, wananchi hao wameitaka Serikali kuhakikisha kuwa fedha zinazotengwa katika bajeti hiyo zinafika kwa wakati na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta matokeo chanya kwa wananchi wa kawaida.

Sauti ya wananchi

Katika hatua nyingine, mwanahabari wetu Samwel Mpogole amefanya mahojiano maalum na mchambuzi wa masuala ya siasa, diplomasia na uchumi Afrika Mashariki, Alex Chigaitan Mwagile, ambapo mwanzo alitaka kufahamu bajeti hiyo ina maana gani kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Sauti ya Mwandishi wetu na Mchambuzi Alex Mwagile

Ikumbukwe kuwa bungeni jijini Dodoma siku ya jana, Juni 12, ilisomwa rasmi bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, ikiwa ni muendelezo wa jitihada za serikali katika kuimarisha uchumi na ustawi wa wananchi.