Highlands FM
Highlands FM
9 June 2025, 17:46

Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato washauriwa kujikita katika Maandiko na maombi ili kuimarika kiroho.
Na Samwel Mpogole
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato wametakiwa kujikita katika kusoma Neno la Mungu na kufanya maombi kwa bidii ili kuimarika kiroho na kuendelea kutembea katika misingi ya imani yao.
Wito huo umetolewa na Mchungaji wa mtaa wa Ruanda, Christopher. Mkama, wakati wa ibada maalum ya Sabato iliyofanyika katika Kanisa la Mbeya Kati, ambapo amewahimiza waumini kuwa na nidhamu ya kiroho kwa kusoma Maandiko Matakatifu kila siku. Akizungumza katika ibada hiyo, Pst. Mkama amegawa gazeti maalum kwa washiriki, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha usomaji wa Neno la Mungu miongoni mwa waumini.
Kwa upande wao, baadhi ya waumini waliopokea gazeti hilo na kushiriki katika ibada hiyo wameonesha kufurahishwa na hatua hiyo, wakisema itawasaidia kuimarika zaidi katika safari yao ya kiroho.
Ibada hiyo maalum ilihudhuriwa na waumini kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya, huku ujumbe mkuu ukiwa ni “Kushiriki Sikukuu ya Vibanda (Makambi)” kama msingi wa maisha ya kila Mkristo katika kumsifu na kumtukuza Mungu kwa moyo na roho.