Highlands FM

Wanaosambaza bidhaa bandia kukiona

30 May 2025, 12:45

Mkuu wa FCC kanda Dickson Mbanga. Picha na Samwel Mpogole

Wanaojihusisha na uuzaji pamoja na usambazaji wa bidhaa bandia kuchukuliwa hatuakali ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani

Na Samwel Mpogole

Serikali imesema haitosita kumchukulia hatua  mzalishaji au msambazaji wa bidhaa yeyote atakayezalisha u kusambaza bidhaa  feki ikiwemo kuingiza nchini kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Akizungumza na Highlands fm Radio katika maonesho ya Mbeya Expo katika viwanja vya uhindini jijini hapa, Mkuu wa kanda wa Tume ya Ushindani (FCC) nyanda za juu kusini Dickson Mbanga, amesema vitendo vya kuuza na kusambaza bidhaa bandia vinadhoofisha ustawi wa taifa na jamii kwa ujumla, hivyo serikali kupitia FCC haiwezi kuvifumbia macho.

Sauti ya Dickson Mbanga

Katika hatua nyingine, Mbanga ametoa wito kwa wananchi kujitokeza katika ofisi za FCC za kanda kupata elimu ya namna ya kutambua bidhaa bandia, akibainisha kuwa tume hiyo inaendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuwajengea uwezo wa kujilinda dhidi ya bidhaa zisizo halali.

Sauti ya Dickson Mbanga

Kwa upande wake, Andason Luiza, Mkaguzi na Afisa Mdhibiti wa FCC , amefafanua kuhusu sheria zinazomgusa mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na biashara au usambazaji wa bidhaa bandia. Amewatahadharisha wahusika kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Sauti ya Andason Luiza

FCC imesisitiza kuwa mapambano dhidi ya bidhaa bandia ni jukumu la kila mmoja, hivyo ushirikiano wa wananchi ni muhimu ili kulinda afya, usalama na uchumi wa taifa.