Highlands FM
Highlands FM
22 May 2025, 13:50

Serikali mkoani Mbeya imeagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU, ishirikiane na Mrajisi Msaidizi wa vyama vya ushirika kuwachukulia hatua viongozi wa vyama vya ushirika wa akiba na mikopo, saccos, ambao wamefuja fedha kwenye vyama vyao na kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa kwa wanachama ili zitumike kuwaletea maendeleo.
Na John ilomo
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa mbeya, Dkt. Juma Zubery Homera wakati akifungua jukwaa la ushirika la mkoa wa Mbeya ambalo linafanyika kwa siku tatu jijini Mbeya
Wakizungumzia ubadhirifu wa mali za ushirika, wasimamizi wa ushirika ngazi ya kitaifa na mkoa wa Mbeya nao wakawa na haya ya kusema
Mwenyekiti wa jukwaa la ushirika mkoa wa Mbeya, Bw. Obed Mtweve amesema pamoja na hatua zinazochukuliwa na serikali kudhibiti ubadhilifu kwenye ushirika, walinzi wa kwanza wa mali za ushirika ni wanaushirika wenyewe, huku baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika wakiomba wapewe elimu zaidi ya kuendesha vyama hivyo.