PCT yawanoa mawakala kuelekea msimu mpya wa mavuno
7 June 2024, 17:03
Na Lameck Charles
Highlands Fm Radio
Kampuni ya Pareto Tanzania (PCT) imewapa mafunzo mawakala wa kampuni hiyo ikiwa ni maandalizi kabla ya kuanza Rasmi Kwa mavuno
Mafunzo hayo yaliyofanyika eneo la Ilembo umalila yamewakutanisha mawakala,wakulima waweze kupata elimu ni maua gani ambayo ni bora kwa kuvuna ili kuweka ubora wa zao hilo.
Kwa Upande wake Gerad Joseph ambye ni afisa kutoka kampuni ya pareto Tanzania (PCT) amesema kwa msimu kwa 2022/23 kamapuni hiyo ilipata hasara ya zaidi ya shilingi billion1 huku akiishukuru serikali ya mkoa wa mbeya kwa kuweka utaratibu kwa kila kampuni ya ununuzi wa pareto kutonunua maua yasiyo bora.
Mussa Malubalo ni Afisa Pareto Mkoa wa Mbeya na Songwe amesema wao kama PCT wamekuwa wakiwapa mafunzo wakulima Kabla ya kuanza Kwa Msimu Ili kuepuka kupata maua yasiyo Bora kama ilivyotokea kwa mwaka jana.
Kampuni ya Pareto Tanzania (PCT) imewakutanisha mawakala wake na wakulima Toka mikoa ya Mbeya na Songwe ikiwa ni Utekelezaji wa Makubaliano yaliyotolewa hivi Karibuni na Serikali ya Mkoa wa Mbeya.