Pambazuko FM Radio

Mbunge Mlimba ataja miradi iliyotekelezwa hadi sasa, inayotekelezwa

23 July 2024, 4:41 pm

Picha ya Mbunge wa Jimbo la Mlimba Mh Godwine Kunambi akiwa studio za Pambazukofm[Picha na kuruthum Mkata]

“wakati  napata  ubunge tatizo la upatikanaji wa maji katika jimbo la Mlimba lilikuwa kubwa sana ukilinganisha na sasa”Mbunge wa jimbo la mlimba godwine Kunambi

N a Elias Maganga

Kampeni ya kumtua mama ndoo kishwni KATIKA Jimbo la mlimba Wilayani kilombero imetekelezwa hadi sasa kwa asilimia 70.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa jimbo hilo Mh Godwine Kunambia alipokuwa akizungumza na pambazukofmkwenye kipindi cha jioni leo july 22 mwaka huu ambapo amesema kuwa wakati  anapata  ubunge tatizo la upatikanaji wa maji katika jimbo hilo lilikuwa kubwa sana ukilinganisha na sasa.

Mh Kunambi amesema awali kulikuwa na kesi nyingi za watu kunywa maji yasiyo salama ,watu kuliwa na mamba mitoni wakati wakitafuta maji alipoingia bungeni alijenga hoja ya kuishawishi serikali wananchi wapate maji safi na salama na serikali imesikia kilio chake na kuanza kutekeleza kwa vitendo ambapo kuna miradi ya maji maeneo mbalimbali ya jimbo hilo inatekelezwa mikubwa kwa midogo.

Amesema tayari Serikali imetoa fedha katika baadhi ya maeneo ya jimbo la mlimba kata ya idete Kijiji cha miwangani kuna mradi wa maji na tayari a kisima kimechimbwa baadae watapeleke mabomba hadi mwishoni mwa mwaka huu wananchi wa maeneo hayo wataakuwa wamepata maji safi na salama

Sauti ya mbunge Godwine Kunambi akielezea miradi ya maji katika JImbo la Mlimba

Pia Mbunge kunambi hakusita kuzungumzia miradi mingine mikubwa inayotekelezwa katika jimbo hilo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa baraabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa km100kanzia  Lumemo darajani Hdi Mlimb na tayari wakandarasi wako site mkandarasi wa kwanza anajenga barabara km62.5 kutoka ifakara hadi igima na mkandarasi mwingine amepewa km 37.5 kuanzia igima hadi chita,barabara hiyo kwa kiwango cha lami inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 36na kinachosubiriwa serikali iwalipe wakandarasi hao wawili malipoa ya awali   {advance payment}na baada ya hapo wakandarasi wataanza kazi

Picha ya bunge wa Jimbo la Mlimba Mh Godwine Kunambi{Piicha na Kuruthum Mkata}
sauti ya mbunge Kunambi akielezea mradi wa barabara kutoka ifakara kwenda mlimba kwa kiwango cha
lami

Mbali na barabara hiyo pia barabara nyingine ni ya kuiunganisha mkoa wa morogoro na mkoa wa njombe yenye urefu wa km 93 kutoka kihansi hadi madege mpakani mwa Njombe na mKoa wa morogoro .

Amesema dhamira ya serikali ni kuunganisha Mkoa wa Morogoro na mkoa wa Njombe kwa kiwango cha lamikwani barabara hiyo ikifunguka uchumi wa waanachi wa Kilombero na Mlimba utakuwa

Saut ya Mbunge Kunambi akielezea barabra ya kuunganisha Mkoa wa morogoro na mkoa wa Njombe