Mkoani FM
Mkoani FM
22 July 2025, 2:58 pm

Tume huru ya taifa ya uchaguzi (INEC) imewataka wasimamizi na wasimamizi wa uchaguzi kufuata sheria katika kutimiza majukumu yao.
Amina Massoud Jabir
Waratibu, wasimamizi na wasaidizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo wametakiwa kufanya kazi zao kwa kufuata sheria, kanuni na miongozo ya tume huru ya taifa ya uchaguzi ili kuepusha kuwa chanzo cha migogoro wakati wa uchaguzi.
Wito huo umetolewa na Makamo Mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania, Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania Mbarouk Salim Mbarouk katika ukumbi wa kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi Chake chake Pemba wakati akifunguwa mafunzo kwa watendaji hao.
Amesema kama ilivyo kuwa uteuzi wao umezingatia sheria za Uchaguzi kifungu namba 6 (1) na kifungu cha 8 na(1) na (2) cha sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Mdiwani namba 1 ya mwaka 2024 hivyo ni muhimu nao kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria hiyo.
Ameeleza kuwa watendaji hao wanawajibu wa kusimamia na kuratibu shughuli za Uchaguzi kwa uadilifu , uaminifu, Uzalendo uchapazi uliotukuka.
Katika hatua nyengine amewataka watendaji hao kuvishirikisha vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili katika hatua zote sambamba na kuwashirikisha wadau wa Uchaguzi kwamujibu wa katiba , Sheria , kanuni, miongozo na maelekezo mbalimbali yaliotolewa na yatakayotolewa na Tume.
Kwa upande wake Hakimu wa Mahakama ya mwanzo Chake Chake Nassor Suleiman Nassor baada ya kuwalisha viapoa amewasihi watendaji hao wa Uchaguzi wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kutokuwa Chanzo cha uvunjifu wa amani na wafanyekazi kwa uadilifu ili kuondowa malalamiko yasiokuwa ya lazima kwa wadau wa Uchaguzi.
Hata hivyo kaimu mkurugenzi Tume huru ya taifa ya Uchaguzi Zanzibar, Adama Mkina amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo maofisa mbali mbali wa Uchaguzi ili waweze kufanya kazi hiyo kwa mujibu wa Sheria na katiba ya nchi ili Uchaguzi huo uwe huru na haki.
Mafunzo hayo yalioratibiwa na tume huru ya taifa ya uchaguzi INEC yamehusisha washiriki 59 wakiwemo Waratibu, wasimamizi wa Uchaguzi na wasimamizi wasaidizi ngazi ya jimbo huku kauli mbiu ya uchaguzi mwaka 2025 “kura yako haki yako jitokeze kupiga kura”