Mkoani FM
Mkoani FM
22 July 2025, 12:47 pm

Wahitimu wa kidato cha nne na cha sita kisiwani Pemba wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujiunga na chuo cha Abdurahman-Alsumait.
Amina Massoud Jabir
Wahitimu wa kidato cha nne na cha sita kisiwani Pemba wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujiunga na chuo cha ABDULRAHMAN-ALSUMAIT kilichopo chukwani Mkoa wa Mjini Magharib Unguja ili kujiendeleza kielimu.
Wito huo umetolewa na Abdulswamad Juma Hamad afisa masoko kutoka chuo cha AbdulRhaman ALSUMAIT wakati akizungumza na Mkoani fm, amesema ni wakti kwa wanafunzi walio maliza masomo yao ya kidato cha nne na kidato cha sita walio na vigezo kuchanagamkia fursa hiyo.
Ameeleza wazazi na walezi wanawajibu wa kushajihisha watoto wao kujiunga na chuo hicho ili kujiendeleza kielimu kwani chuo hicho kina walimu wazoefu na wenye kiwango cha juu katika usomeshaji.
Akitaja vigezo vinavyotumika kusajili wanafunzo katika chuo hicho afisa udahili Is-haka Mbwana Othman amesema, kwa ngazi ya cheti kwa mwanafunzi aliemaliza kidato cha nne awe na ufaulu wa D 4 ukitoa ya dini, diploma, degree pamoja na master.
Akitaja kozi zinazotolewa kwa upande wa cheti na diploma ni usimamizi wa ofisi, Pamoja saikolojia ya ushauri nasihi, kwa upande wa digree uwalimu wa sana na sayansi, saikolojia ya ushauri nasihi, teknolojia ya Habari na mawasiliano na master ya sheria na fiqhi ya kiisilam .
Kwa upande wake mkufunzi Muslim Hijja Abdulmalik amewatoa hofu wazazi Pamoja na wanafunzi wanaotaka kujiunga na chuo hicho kwa kusema chuo kinafuata maadili, ubunifu pamoja na ujasiriamali.