Mkoani FM
Mkoani FM
25 June 2025, 12:52 pm

Jamii nchini imetakiwa kutumia nishati mbadala kwa ajili ya kutunza mazingira na kulinda afya za watumiaji.
Hayo yameelezwa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ismail Ali Ussi, wakati akitoa salamu za mwenge katika shehia ya Mkanyageni sambamba na kukabidhi majiko ya gesi kwa baadhi ya wanachi wa shehia hio.
Amesema wamefika katika shehia ya Mkanyageni kujionea namna baraza la mji na serekali ya wilaya wanavyoendeleza hamasa juu ya matumizi ya nishati mbadala ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya matumizi ya nishati mbadala ilioanzishwa na viongozi wakuu wa kitaifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Hamad Omar Bakar amesema utoaji wa majiko hayo kwa baadhi ya wananchi ni chachu ya matumizi ya mishati mbadala na kuacha matumizi ya nishati chafu ya kupikia pia amewataka wanchi waliopata majiko hayo kua mabalozi wazuri wa matimizi ya nishati mbadala.

Mapema akisoma risala mbele ya kiongozi wa mwenge kitaifa Mohammed Juma asemesema matumizi ya nishati mbadala yatapunguza matumizi ya ukataji wa miti na uharibifu wa mazingira ambayo yanapelekea mabadiliko ya tabianchi.
Jumla majiko 50 yenye thamani ya shilingi milioni mbili laki mbili ishirini na saba elfu mia saba na sabiini yametolewa na kukabidhiwa kwa wananchi.