Wakulima Pemba watakiwa kulima kilimo hai
30 November 2024, 11:54 am
Wakulima kisiwani Pemba wameshauriwa kujikita kwenye kilimo hai kwani ni rahisi na kinasaidia kuondokana na umasikini na kuleta mafanikio kiuchumi
Wakizunguma na Mkoani FM, wakulima Bi Salama Omar na Zainab Rajab wamesema kilimo hicho mali ghafi zake ni rahisi ukilinganisha na kilimo kingine na kinalinda afya zao kutokana na kutotumia mbolea zenye sumu hali inayopelekea kujipatia kipato kwa haraka.
Bwana Shamba kutoka Milele Zanzibar Foundation Abdallab Omar Sheha amesema kilimo hai kinasaidia kulinda ardhi kutokana na athari ya mabadiliko ya tabianchi.
Mkuu wa Idara ya Kilimo na Uhakika wa Chakula Bi. Asha Omar Fadhili amesema mtazamo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuhamasisha wakulima kulima kilimo hai ili kupunguza utumiaji wa kemikali kwenye mazao na kulinda afya za walaji.