Mkoani FM
Makoongwe Pemba walia kukosa maji safi na salama zaidi miaka minne
30 November 2024, 8:29 am
Ukosefu wa maji safi na salama katika kisiwa cha Makoongwe hasa vijiji vya Kinyasini na Kizambarauni ni changamoto inayozorotesha shughuli zao za kiuchumi
Wakizungumza na Mkoani FM Saumu Abas Mohd Ali na Rukia Omar wamesema ni mwaka wa nne sasa tangu kukosekana kwa maji hayo hali inayowalazimu kufuata huduma hiyo umbali mrefu kwa ajili ya shughuli zao.
Haji Omar Haji sheha wa Shehia ya Makoongwe amesema.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano Mamlaka ya Maji (ZAWA) Suleiman Anasa Masoud amesema wanafahamu changanoto ya maji katika kisiwa cha Makoongwe kama anavyoeleza
Kisiwa cha Makoongwe kina zaidi ya wakazi 2,200, na shughuli kubwa ni uvuvi, kilimo na ufugaji na shughuli zote zinahitaji huduma ya maji.