Mkoani FM

Panza wanufaika na uhifadhi wa eneo la bahari

26 May 2024, 9:42 pm

Haji khatib Haji afisa tathmini na ufuatiliaji wizara ya uchumi wa buluu (Picha na Khatib Nahoda)

Iwapo wanawake watapewa nafasi katika uhifadhi wa mazingira ya bahari wanaweza kua mabalozi wazuri kwa kuwalea vijana na kuwapa elimu ya uhifadhi wa mazingira hayo.

Na Khatib Nahoda

Jamii nchini imetakiwa kuwashirikisha wanawake katika shughuli za uchumi wa buluu Ili kufikia azma ya serikali kuinua kipato cha kundi hilo.

Hayo yamesemwa na Haji khatib Haji Afisa tathmini na ufuatiliji wizara ya uchumi wa buluu kwa niyaba ya afisa mdhamini wa wizara hio wakati wa ufunguzi wa hifadhi ya Pweza na viumbe vyengine vya baharini huko kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba.

Amesema iwapo wanawake watapewa nafasi katika uhifadhi wa mazingira ya bahari wanaweza kua mabalozi wazuri kwa kuwalea vijana na kuwapa elimu ya uhifadhi wa mazingira hayo.

Aidha amesema azma ya serekali ni kuongeza idadi ya wanawake kwenye shughuli za uchumi wa buluu na kuinua kipato chao kwani asilimia zaidi ya 50 ya watu wote ni wanawake.

Sauti ya Haji khatib Haji Afisa tathmini na ufuatiliji wizara ya uchumi wa buluu

 Aisha Abadalla Rashid Mkuu wa kitengo cha elimu ya mazingira Pemba amesema uhifadhi huo unatokana na mradi wa safaya unaosimamiawa na afisi ya makamo wa kwanza wa raisi, lengo kuu ni uhifadhi wa ikolojia ya ukanda wa bahari ya Kisiwa cha Pemba, kuinua wanachi kiuchumi na kukabiliana na mabadidiliko ya tabinchi.

Sauti ya Mkuu wa kitengo cha elimu ya mazingira Pemba Aisha Abadalla Rashid

Akielezea changamoto katika ufungiaji huo Mjumbe wa kamati ya uvuvi wa kisiwa hicho Miraji Ali Shaali amesema ni baadali ya walinzi kutokuhudhuria katika eneo la hifadhi ipaswavyo.

Kwa upande wao wavuvi Juma Ngwali Makame na Amina Gharib Issa wamesema walikubaliana kuhifadhi kwa kufungia eneo hilo baada ya kuona kipato chao kimeshuka kutokana na mazao ya baharini.

Sauti za wavuvi wa pweza kisiwa panza Juma Ngwali Makame na Amina Gharib Issa

Hifadhi hiyo ya kisiwa Panza imefungiwa kwa muda wa miezi 4 kutoka Januari hadi Mai 2024 na wastani wa kilo 217 kwa siku ya kwanza zimevuliwa  na  wavuvi watavua kwa siku 4 na kufungiwa kwa mara nyengine.