Pemba kusogezewa mahakama ya rufaa
25 May 2024, 6:39 am
Jaji mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan amesema mahakama kuu ya Tanzania imedhamiria kujenga kituo jumuishi kisiwani Pemba ili kukidhi haja na matakwa ya wananchi kisiwani humo.
Ameyasema hayo mara baada ya utiaji wa Saini mkataba wa ujenzi kati ya mahakama kuu ya Tanzania na kampuni ya ujenzi ya Deep construction Limited, utakao gharim shilingi bilioni 9.7 na utachukua miezi tisa hadi kukamilika kwake.
Kwa upande wake Kai Rashid Mbarouk mtendaji mkuu wa mahakama ya Zanzibar amesema ujio wa mahakama hiyo ni kuwapunguzia shida na kadhia ilokuwa ikiwakabili wananchi wa Pemba na kutoa nafasi ya mazingira bora ya kufanyia kazi kwa watendaji wa mahakama wakiwemo majaji mahakimu na watendaji wengine.
Mtendsaji mkuu wa mahakama Tanzania Elisante Gabriel ameeleza lengo la ujio wa kituo hicho ni kutoa fursa kwa watu wa Pemba kupata huduma za kituo jumuisha ambacho kinazingatia huduma kwa watu wote lakini pia kushajihisha muktadha wa muungano wa Tanzania.
Msajili mkuu wa mahakama Tanzania Eva Nkya amesema mahakama hiyo ya rufaa imekuja kupunguza gharama kwa wanachi wa Pemba kufuata huduma za kimahakama na kuwafanya waendelee kufanya shughuli nyengine za ujenzi wa taifa.
Kwa upande wake mkandarasi wa mradi huo Ravinda Singh Jabbal kutoka kampuni ya Deep Construction Limited ameahidi kumaliza kazi hiyo kwa wakati uliowekwa na kuwaomba wananchi wa Pemba kutoa mashirikiano ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
Bimkubwa RajabTangwi sheha wa mfikiwa amemuomba mkandarasi huyo kutoa kipaoumbele cha ajira kwa vijana wa shehia hiyo ili kuuunga mkono ujenzi huo.
Ghafla ya utiaji Saini kati ya mahakama kuu Tanzania na kampuni ya M/s Deep Construction Limited imefanyika katika ukumbi wa ZRA Gombani chake chake Pemba na utagharimu shilingi bilioni 9.7 fedha hizo ni kati za mkopo wa mahakama ya Tanzania iliyopatiwa kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza ni dola milioni 65, na milioni 90 ambapo zimejumuisha kujenga vituo jumuishi 9 kikwemo cha mfikiwa na mahakama za mwamzo 60 hadi kukamilika kwake na unatarajiwa kuchukua miezi tisa ya ujenzi kuanzi siku ya utiwaji Saini hadi February 2025.