Early Madrasa Childhood: Kuwapa elimu ya utetezi watu wenye ulemavu
26 November 2022, 8:38 am
Watu Wenye Ulemavu Kisiwani Pemba wamesema elimu waliyopatiwa kutoka taasisi ya Early Madrasa Childhood imeweza kuwasaidia kuwajengea uwelewa wa kiutetezi katika kupata haki zao kisheria.
Akizungumza Maryam Juma Kombo kutoka Taasisi ya Usalama Barabarani amesema kupitia elimu hiyo ameweza kujiamini zaidi ukilinganisha na hapo awali jambo linalosaidia katika harakati zake za kila siku.
Saida Amour mratibu wa mradi wa Maendeleo Jumuishi ya Jamii Community Based Inclusive Development (CBID) kutoka Early Madrasa ChildHood amesema lengo la mradi huu ni kuongeza uwelewa kwa watu wenye ulemavu juu ya simamia haki zao za msingi katika nyanja mbalimbali.
Salma Haji Sadati mkufunzi Mkuu wa mradi katika kuwajengea watu wenye ulemavu amesema Misingi ya maendeleo ni uchambuzi wa Sera na Sheria hivyo ni vyema kwa waliopata fursa ya kufikiwa na elimu hii waitumie vizuri lengo ni kuona kwa namna gani yale yaliyosahauliwa yanawafikia na kupata ushawishi wa kiutetezi.
Simon Meigaro Moikan Mkurugenzi Mkaazi kutoka shirika la Agakhan Tanzania amesema shirika limeweza kuiwezesha taasisi ya Early ChilHood kuwafikia kundi hilo lengo ni kuongeza nguvu katika kulifikia kundi hilo kwa njia jumuishi ili watu wenye ulemavu kupatiwa fursa sawa kwenye harakati za maendeleo.
Malengo17 ya Dunia ya maendeleo endelevu ameeleza kuwa ushawishi na utetezi wa haki za watu wenye Ulemavu na kupata fursa sawa kama watu wengine hapa visiwani Zanzibar