Mkoani FM

Mrajisi: Wafanyabiashara kateni rufaa kupitia baraza la ushindani halali wa biashara Zanzibar

1 September 2022, 11:01 am

Mrajisi wa baraza la ushindani Halali la biashara Zanzibar Fatma Gharib Haji

Wafanya biashara wilaya ya mkoani wametakiwa kutumia fursa za kukata rufaa kupitia Baraza la ushindani halali wa biashara Zanzibar ili kupata haki zao kisheria endapo hawakutendewa haki na watoa huduma mbalimbali Zanzibar .

Hayo yameelezwa na mrajisi wa baraza hilo Fatma Gharib Haji huko katika ukumbi wa mkoani hotel katika warsha ya siku moja yakuzungumza na wafanyabiashara sambamba na wasaidizi wa sheria lengo ni kuwawezesha wanajamii kutumia huduma ya Rufaa inayopatikana kwenye barazani hapo.

Ameeleza jamii na wafanya biashara watumie fursa iliopo kwenye baraza hilo ili kufikisha malalamiko yao ya kukata rufaa lengo kupatiwa haki katika masuala ya ushindani kwani serikali ni kumlinda mtumiaji wa bidhaa na mfanyabiashara katika harakati za ukuwaji wa uchumi.

Abass Juma Fakih Kaimu mkurugenzi idara ya mashauri amesema ni vyema kwa wafanya biashara kutumia baraza hilo na sio kuelekea mahakamani kwa utatuzi au kupatiwa haki endapo watakumbana na changamoto za kibiashara

Akitoa shukrani kwa niaba ya washiriki Nassor Hakim msaidizi wa sheria wilaya ya mkoani amesema kupitia taasisi yake mafunzo hayo yatasaidi katika kuifikia jamii zaidi aidha amesema ni vyema taasisi zinazolalamikiwa kutoa elimu kwa jamii ili waweze kudai haki zao kisheria.

Sharia namb. 5 ya baraza la ushindani halalai wa biashara Zanzibar ya mwaka 2015 imetoa fursa za kuanzishwa kwa jumuiya za watumiaji wa huduma ili kuwasaidia kuwafikishia malalamiko yao sehemu husika, aidha kifungu namb.32(1)kimeeleza majukumu ya baraza na kif 34(1) cha baraza hilo.