Wizara ya afya watakiwa kutoa elimu ya chanjo vijijini
9 October 2021, 8:14 am
Kutokuwepo kwa elimu ya kutosha kwa baadhi ya vijiji ni changamoto inayopelekea kushindwa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa korona.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti wananchi wa wilaya ya mkoani wamesema ni vyema wizara ya afya iweke utaratibu wa kuwafikia wananchi hususani wa vijijini ili kuwapatia elimu hiyo .
Kwa upande wao baadhi ya masheha wamesema ipo haja kwa jamii kupatiwa elimu ya kujilinda na corona ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza.
Afisa Mdhamin wizara ya Afya Pemba Yakuob Mohammed Shoka amesema wamejipanga kutoa elimu kwa kushirikiana na kitengo cha elimu ya afya kwani bado wanakazi kubwa ya kuelimisha jamaii juu ya wimbi la tatu la korona na kuitaka jamii kuwa tayari kufuata yale maelekezo yote wanayopewa na wataalamu wa afya.
Sambamba na hayo wameiomba wizara husika kupatiwa elimu ya ugonjwa huo ili waweze kushirika kikamilifu ktika zoezi hilo bila ya kuwa na hofu.