Highlands FM

Taweru watoa msaada kwa wanawake gereza kuu Ruanda Mbeya

18 March 2026, 09:24

Wanawake wa chama cha wakusanya mapato Tanzania { TAWERU} wakikabidhi vitu mbalimbali kwa mkuu wa gereza ruanda mbeya kwa ajili ya wanawake walioko gerezani.

Chama cha Wafanyakazi waKusanya Mapato Tanzania, TAWERU, kimetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wanawake walioko katika Gereza Kuu la ruanda mkoani Mbeya, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, huku kikitoa wito kwa jamii kuwajali na kuwasaidia watu wenye uhitaji

Na Mwanaisha Makumbuli

Chama cha Wafanyakazi wakusanya Mapato Tanzania (TAWERU) kimetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wanawake waliopo katika Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa wa kamati ya Wanawake wa chama cha wakusanyamapato Tanzania ngazi ya Taifa wa TAWERU, Jennifer Melani Mathias, amesema lengo la msaada huo ni kuonyesha mshikamano na kuwajali wanawake walioko magerezani, huku akiwahimiza wadau na wananchi kujitokeza kusaidia makundi yenye uhitaji katika jamii.

Sauti ya Jennifer Melani Mathias

Kwa upande wake, Mkuu wa Gereza Kuu la Ruanda, Kamishna Msaidizi wa Magereza Christopher Fungo, ameishukuru TAWERU kwa msaada huo ambao umejumuisha vitu mbalimbali ikiwemo taulo za kike kwa ajili ya wafungwa wanawake.

Sauti ya Christopher Fungo

Naye Katibu wa Kamati ya Wanawake Taifa wa TAWERU Dorothy Msofu, amesema shughuli hiyo inalenga kuwakumbuka wanawake walioko magerezani na kuwahakikishia kuwa bado ni sehemu ya jamii na wanapaswa kupewa msaada na faraja.

Sauti ya Dorothy Msofu

Jamii inapaswa kubadili mtazamo na kujenga utamaduni wa kuwatembelea na kuwajali wafungwa pamoja na mahabusu walioko magerezani ili kuwapa faraja na matumaini ya maisha.