Highlands FM
Highlands FM
6 March 2026, 12:26

Watumishi wa umma wametakiwa kuzingatia maadili ya kazi na kujiepusha na vitendo vya ulevi vinavyoweza kusababisha uvujaji wa siri za ofisi pamoja na kudhoofisha taswira ya taasisi na serikali kwa ujumla.
Na Isack Mwashiuya
Watumishi wa umma wametakiwa kuzingatia maadili ya kazi ikiwamo kuachana na ulevi sababu inayoweza kepelekea kuvujisha siri za ofisi.
Hayo ni kwa mujibu wa Enock mwaitebele Ofisa kutoka Sekretarieti ya maadili maadili ya viongozi wa umma wakati akiwasilisha mada kuhusu mfumo wa ujazaji wa Tamko la rasilimali na madeni kwa njia ya mtandao (online declaration system) katika mafunzo ya maadili kwa wakuu wa idara na vitengo vya tehama kutoka taasisi za umma na wizara Mkoa wa mbeya ,mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Mbeya machi 5 2026.
Mwaitebele ameongeza kuwa suala la ulevi si tu hujenga taswira mbaya kwa mtushi binafsi bali kwa taasisi anayofanyia kazi na serikali kwa ujumla.
Kwa upande wake katibu msaidizi sekretariet ya maadili nyanda za juu kusini Bw Paul Kanoni ameelezea lengo la mafunzo hayo kwa taasisi na wakuu wa idara
Baadhi ya washiriki wameeleza juu ya manufaa waliyopata katika mafunzo hayo huku wakibainisha kuwa watakwenda kuwa mabarozi na waalimu kwa watumishi wengine katika taasisi wanazofanyia kazi.
Mafunzo hayo yanakuja wakati ambao mifumo mbalimbali ya kiserikali huendeshwa kwa mfumo wa kidigitali ambapo huwataka watumishi wa umma kutumia mifumo hiyo katika kutoa huduma kwa wananchi sambamba na kujaza taarifa zao binafsi kwa matumizi ya kiofisi na kiserikali.
